Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania (TCAA), imepiga marufuku urushwaji angani wa vifaa vya kieletroniki visivyo na rubani (drones) bila kupata kibali maalum cha mamlaka hiyo.
Taarifa iliyotolewa kwa umma na kusainiwa na Mkurugenzi Mkuu wa TCAA, Hamza Johari imeeleza kuwa kuanzia sasa kwa taasisi au mtu binafsi kufanya majaribio, anayetaka kununua au kurusha drones, ni lazima apate idhini ya Wizara ya Ulinzi na Usalama husika pamoja na Mamlaka hiyo.
Pia uendeshaji wa shughuli zote za anga nchini uko chini ya Mamlaka hiyo kwa mujibu wa sheria na kanuni zilizopo.
Kwa sasa hapa nchini drone zimekuwa zikitumika kwa ajili ya kupiga picha za angani maeneo ya mashamba makubwa, mkusanyiko mkubwa wa watu. Pia zimekuwa zikitumika mara nyingi katika kuandaa video za muziki.
Title :
TCAA yakataza matumizi ya drones bila kibali
Description : Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania (TCAA), imepiga marufuku urushwaji angani wa vifaa vya kieletroniki visivyo na rubani (drones) bila kup...
Rating :
5