Baada ya choko choko za kila mara kutoka kwa Gigy Money kwenda kwa msanii Shilole, hatimaye msanii huyo ameonyesha kuchukulia poa choko choko za video vixen huyo.
Siku zilizopita Gigy Money alidai hawezi kufanya muziki na Shilole kwa sababu hamshabikii na hajawahi kupenda muziki wake, pia hivi karibuni alidai Shilole hajui kuongea kingereza vizuri.
Kupitia 5 Selekt ya EATV Shilole amesema ni kweli hajui kingereza vizuri, na anamchukulia Gigy Money kama mdogo wake.
“Ni mdogo wangu kwa hiyo lazima apite kwa dada yake, kwa hiyo watu kama hao wadogo zangu ninawachukulia poa tu, hamna tatizo,” amesema Shilole na kuongeza kuwa.
“Kingereza is not my language, kwa hiyo nikisema bado hainilazimishi kukijua sana lakini najifunza kuongea, na pale panapobidi nitaongea. Hiyo ni kweli hamna shida kama sijaenda (shule) ni sawa, kwani watu wangapi hawajaenda shule, ukiwa umeenda shule na hela uwenayo,” amesistiza.
Title :
Shilole ‘Ampuuzia’ Gigy Money
Description : Baada ya choko choko za kila mara kutoka kwa Gigy Money kwenda kwa msanii Shilole, hatimaye msanii huyo ameonyesha kuchukulia poa choko...
Rating :
5