Mshindi wa SportPesa Super Cup 2017, Gor Mahia ya nchini Kenya imewasili nchini mchana huu kwaajili ya mchezo wao wa kirafiki dhidi ya klabu ya Everton kutoka nchini Uingereza.
Mchezo huyo utachezwa Alhamisi hii Julai 13 katika Uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam.
Gor Mahia jioni ya leo watatembelea uwanja wa taifa kwaajili ya mazoezi ya mwisho.
Timu ya Everton inatarajiwa kuwasili nchini Jumatano hii huku ikiwa na mchezaji wake mpya, Wayne Rooney waliomsajili kutoka Manchester United.
Tayari homa ya mpambano huo miongoni mwa mashabiki nchini imeendelea kuwa kubwa huku wengi wakiwa na shauku ya kuwaonya nyota mbalimbali wa Everton kama vile Jordan Pickford, Ross Barkley, Idrissa Gana Gueye na wengine wengi.
Viingilio vya mchezo huo ni Sh 8000/= kwa VIP C na Sh 3000/= kwa viti vya mzunguko na mchezo unatarajiwa kuanza majira ya saa 11 jioni. Angalia picha.
Title :
Picha: Gor Mahia watua Bongo kuwavaa Everton
Description : Mshindi wa SportPesa Super Cup 2017, Gor Mahia ya nchini Kenya imewasili nchini mchana huu kwaajili ya mchezo wao wa kirafiki dhidi ya klab...
Rating :
5