Siku ya mtoto wa Afrika ina lengo la kutambua thamani, utu , na umuhimu wa mtoto duniani, mwaka 1991 ndio siku ambayo maadhimisho hayo yalianza baada ya Jumuiya ya Umoja wa Afrika kutangaza kufanyika hilo kila mwaka. Katika kutambua hilo mtoto Ethan Yona amefanya kitu kikubwa kwenye maisha yake katika siku hiyo.
Ethan (Wa mbele aliyevaa nguo nyekundu) akiwa na watoto wenzake katika siku ya mtoto wa Afrika, katika viwanja vya JK Yourth Park
Ethan ambaye ana umri wa miaka sita na anasoma darasa la kwanza, ameweza kutengeneza kitabu kilichokuwa katika mfumo wa game ambacho kinaelezea vitu ambavyo anatamani kuja kuvifanya katika maisha yake ya baadae.
Ndoto hizo za mtoto huyo kufanya hilo lilianza mwaka jana kwa kulifikisha kwa wazazi wake, na wao hawakusita kumsikiliza na kumuunga mkono kwa kile anachokifikiria kwa kumkutanisha na kampuni ya i-Learn East Africa ambao wamemsaidia kuweka mawazo yake katika mfumo wa game ambayo imepewa jina la EthanMan.
“Nimekuwa na juhudi sana, kufurahia kujifunza mambo mapya na kupendelea kucheza game. Siku moja niliwaambia wazazi wangu kwamba ningependa kuunda shujaa wangu ambaye ataendana na sifa zangu. Waliniuliza, ni sifa gani hizo, nikawaambia mimi nina kipaji na ninaweza kuwa kitu chochote, nataka kuwa kama mcheza soka, wanamuziki wa rock, mhandisi nk. na hapo ndipo wazo la tabia ya shujaa mkubwa ikaja,” amesema Ethan.
Wakati huo huo kitabu hicho kimeanza kupatikana mtandaoni.
Title :
Mtoto Ethan Yona azindua kitabu kinachoelezea maisha yake
Description : Siku ya mtoto wa Afrika ina lengo la kutambua thamani, utu , na umuhimu wa mtoto duniani, mwaka 1991 ndio siku ambayo maadhimisho hayo yal...
Rating :
5