Muda mfupi baada ya msanii wa kitambo kwenye muziki wa kizazi kipya Bongo, Afande Sele kusikika kwenye kituo kimoja cha redio akitoa maneno ya kuudhi kwa wasanii Vanessa Mdee ‘Vee Money’ na Man Fongo, mwanadada huyo ameshindwa kuvumilia na kujibu mapigo kwa mafumbo.
Katika intavyuu hiyo, Afande Sele anasikika akimnanga Vanessa kwamba muziki wake anakopi sana kutoka Marekani, kuanzia sauti, mashairi, mavazi mpaka video, na kusema hawezi kuwa wa kimataifa kama ‘media’ zinavyomnadi, ukimlinganisha na mwanamama Saida Karoli ambaye muziki wake ulikuwa na vionjo vya Kitanzania.
Kupitia Twitter, Vanessa ambaye anafanya vizuri na wimbo wa ‘Duasi’ alioshirikishwa na Legendary Beatz akaandika ujumbe ambao japo hakuandika amemlenga nani, moja kwa moja ulionesha kuwa ni majibu ya kile kilichosemwa na Afande Sele. Tazama alichokiandika
Mwaka huu umeendelea kuwa mwaka wa mafanikio ya kupanda zaidi katika ngazi za kimataifa kwa Vee Money, ingawa amekuwa akikumbana na changamoto kadhaa ikiwa ni pamoja na kutajwa kwenye orodha ya wasanii waliotuhumiwa kujihusisha na madawa ya kulevya.
Msanii huyo ameendelea kukubalika ndani na nje ya nchi ambapo amekuwa akipewa mashavu kadhaa kung’arisha nyimbo za wasanii wa nchi za Afrika Kusini na Afrika Magharibi.
Title :
Vanessa Mdee Alalamika Kuchafuliwa na Afande Sele
Description : Muda mfupi baada ya msanii wa kitambo kwenye muziki wa kizazi kipya Bongo, Afande Sele kusikika kwenye kituo kimoja cha redio akitoa ...
Rating :
5