MBAO FC.
MATUMAINI ya Simba na Yanga kushiriki michuano ya kimataifa mwakani yapo shakani baada ya vijana hao wa mtaa wa Twiga na Jangwani kukubali kipigo cha bao 1-0 dhidi ya Mbao FC kwenye mechi ya nusu fainali iliyopigwa Uwanja wa CCM Kirumba jana.
Bao la kujifunga la Andrew Vincent katika dakika ya 28 wakati akiokoa shuti lililochongwa na wingi ya kulia na Pius Mswita, ndilo lililoiangamiza Yanga na kuifanya moja kwa moja nayo kupoteza nafasi ya kushiriki Kombe la Shirikisho barani Afrika hapo mwakani, hivyo sasa matarajio yao kubaki katika kutwaa ubingwa wa Ligi Kuu Bara ili kuweza kushiriki michuano ya kimataifa mwakani.
Kutolewa huko kunaiweka Yanga katika wakati mgumu wa kushiriki michuano ya kimataifa kwani kama Simba itatwaa ubingwa wa Ligi Kuu, inamaana Wanajangwani hao wataishia tu kuhesabu ndege zinazotua na kuruka Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA).
Kadhalika, Simba nayo ina wakati mgumu kwani kama ikipoteza mechi ya fainali ya Kombe la FA dhidi ya Mbao FC huku ikiukosa ubingwa, maana yake itarejea tena kuhesabu ndege JNIA tangu ilipoanza kufanya hivyo baada ya msimu wa 2011/12, ubingwa ulipotoweka Msimbazi.
Mshindi wa Kombe la FA, atashiriki Kombe la Shirikisho Afrika wakati bingwa wa Ligi Kuu Bara akiiwakilisha nchi kwenye Ligi ya Mabingwa Afrika.
Simba na Yanga ndizo timu pekee zenye nafasi ya kutwaa ubingwa wa Ligi Kuu Bara, hivyo kama Wanajangwani hao wangeibuka na ushindi jana dhidi ya Mbao FC, ni wazi timu hizo mbili zote zingekuwa zimekata tiketi ya kushiriki michuano ya kimataifa mwakani.
Kwa maana kwamba, kama Simba au Yanga mojawapo ikitwaa ubingwa wa Ligi Kuu, na endapo zingekutana fainali, timu itakayofungwa ingeshiriki Kombe la Shirikisho Afrika kwa kuwa timu moja hairuhusiwi kuiwakilisha nchi katika michuano miwili inayoandaliwa na Shirikisho la Soka Afrika (Caf) kwa msimu mmoja.
Hivyo, ndoto za Yanga kushiriki michuano ya Kombe la Shirikisho Afrika ilipeperuka rasmi jana, lakini Simba bado ina nafasi hiyo pamoja na ile ya Ligi ya Mabingwa Afrika endapo itatwaa ubingwa, wakati Mbao FC nayo ikiwa na matarajio makubwa ya kutaka kukifunga kikosi hicho cha Mcameroon Joseph Omog ili kushiriki michuano ya kimataifa kwa mara ya kwanza katika historia yake.
Simba imetinga katika fainali hizo baada ya kuifunga Azam FC kwa bao 1-0 katika mechi ya nusu fainali iliyopigwa juzi Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.
Kutokana na soka lililoonyeshwa na Mbao FC jana dhidi ya Yanga, Simba ina kibarua kigumu katika mechi ya fainali.
Title :
Simba, Yanga njia panda kimataif
Description : MBAO FC. MATUMAINI ya Simba na Yanga kushiriki michuano ya kimataifa mwakani yapo shakani baada ya vijana hao wa mtaa wa Twiga na Jan...
Rating :
5