Mkurugenzi wa kampuni ya NYEGERAWAITU ENTERTAINMENT, Kampuni inayojihusisha na Sanaa iliyoko Temeke maeneo ya Buza Changulu, amefunguka yamoyoni na kuwaomba wadau wa muziki na sanaa kwaujumla kuwa na upendo na umoja katika sanaa.
NTAMBA ambaye ni mmiliki wa Band inayofanya vizuri kwa sasa inayotambulika kama NTAMBA BAND, aliyasema hayo alipokuwa katika kituo cha radio CITY FM [97.1] juzi jijini Dar es salaam.
Dr. Ntamba aliyasema hayo katika kipindi cha KURASA MSETO baada ya kuulizwa swali na
mtangazaji mmoja wa kipindi hicho;je wewe kama mkurugenzi wa Nyegera waitu umejipanga vipi kuhakikisha kampuni yako inasonga mbele? ndipo alijibu amejipanga vizuri lakini akaomba wadau,mameneja na wakurugenzi wa band na makundi mbalimbali ya sanaa kuwa na upendo na sio kuchukiana,pia akasisitiza na kuwaomba mameneja kutembeleana na kubadilishana mawazo ya kibiashara katika muziki.
By Albert Luhogola
Title :
DR.NTAMBA NA MUNGU_ TUWE NA UPENDO TUSIONEANE WIVU, SANAA INAHITAJI UMOJA
Description : Mkurugenzi wa kampuni ya NYEGERAWAITU ENTERTAINMENT, Kampuni inayojihusisha na Sanaa iliyoko Temeke maeneo ya Buza Changulu, amefunguka ya...
Rating :
5