Wanamuziki machachari wa muziki wa kizazi kipya Naseeb Abdul almaarufu kama Diamond Platnumz na Ally Kiba wamekataa kuimba kolabo ambayo ilitarajiwa kuwa ndio wimbo wa hamasa kwa ajili ya kuhamasisha vijana wa timu ya taifa ya vijana chini ya umri wa miaka 17 Serengeti Boys katika michuano ya vijana Afrika nchini Gabon.
Taarifa hyo imetolewa na Maulid Kitenge katika ukurasa wake wa Twitter, ambaye ni mmoja wa wajumbe wa kamati ya uhamasishaji ya Serengeti Boy, amesema “Kiba na Diamond wameshindwa kuonesha uzalendo kwa Serengeti Boys wamegoma kuimba wimbo wa hamasa licha ya kuwepo kamati ya hamasa, inasikitisha”
Wasanii hao ambao pia ni wajumbe wa kamati ya uhamasishaji ya Serengeti Boys wamefikia uamuzi huo huku wengi wa mashabiki wa muziki wa kizazi kipya na wapenzi wa mpira wa miguu wakitegemea kolabo ya wasanii hao katika wimbo wa kuhamasisha Srengeti Boys. Wasanii hao walitegemewa kuingiza kuimba kolabo hiyo na wasanii wengine ambao ni Darasa, Mwasiti Almas, na Vanesa Mdee
Title :
DIAMOND NA KIBA WAGOMA KUIMBA KOLABO KWA AJILI YA SERENGETI BOYS
Description : Wanamuziki machachari wa muziki wa kizazi kipya Naseeb Abdul almaarufu kama Diamond Platnumz na Ally Kiba wamekataa kuimba kolabo ambayo il...
Rating :
5