Mgombea wa kiti cha urais wa Marekani kwa chama cha Democtaric Bi Hillary Clinton amelitaka shirika la kijasusi la FBI litoe maelezo zaidi kuhusu yaliyomo kwenye barua zake pepe walizonazo FBI.
FBI linasema wanazitumia kuanzisha upya uchunguzi kuhusu iwapo alizembea kwa kutohifadhi vyema taarifa muhimu za kiserikali wakati alipokuwa waziri wa mambo ya nje wa Marekani.
Bi Clinton amesema ana imani kuwa taarifa hizo mpya walizo nazo FBI hazitabadili kivyovyote vile uamuzi wa awali waliotoa hapo July ambao ulimwondolea lawama .
Bi Clinton Amesema, 'Hata hao FBI wenyewe bado hawana hakika iwapo kuna ushahidi mzito kuhusu swala hilo'.
Hata hivyo haijabainika wazi ni kwa kisi gani Ugunduzi wa maelezo hayo unaweza kutetelesha kampeni ya Bi Clinton wakati huu ambapo zimesalia siku 11 pekee , kabla ya uchaguzi huo wa Marekani.
Lakini kama ilivyotarajiwa mpinzani wa Bi Clinton mgombea wa chama cha Republican , Donald Trump, amempiga vijembe upya kinara huyo wa Democrats akisema hapaswi kupeleka kile alichokiita mfumo wake wa kihalifu katika ikulu ya White House.
Title :
Clinton ataka taarifa zaidi kuhusu uchunguzi wa barua pepe zake
Description : Mgombea wa kiti cha urais wa Marekani kwa chama cha Democtaric Bi Hillary Clinton amelitaka shirika la kijasusi la FBI litoe maelezo zaid...
Rating :
5