Mshambuliaji wa kimataifa wa Tanzania, Thomas Emmanuel Ulimwengu ameshindwa kusafiri na timu yake, TP Mazembe ya DRC kwenda Tunisia kutokana na pasipoti yake ya kusafiria kwisha.
Mazembe ilibisha hodi Fainali ya Kombe la Shirikisho Afrika baada ya kulazimisha sare ya 1-1 ugenini dhidi ya wenyeji, Etoile du Sahel katika Uwanja wa Olimpiki mjini Sousse, Tunisia, mwishoni mwa wiki iliyopita.
Ulimwengu amesema amerudi Tanzania kufuatilia pasipoti mpya ya kusafiria, na akiipata atarejea mara moja DRC kujiunga na TP Mazembe.
Title :
Thomas Ulimwengu kuikosa Etoile du Sahel kwa sababu ya 'pasipoti'
Description : Mshambuliaji wa kimataifa wa Tanzania, Thomas Emmanuel Ulimwengu ameshindwa kusafiri na timu yake, TP Mazembe ya DRC kwenda Tunisia kutokan...
Rating :
5