Aliyekuwa makamu wa rais nchini Sudan Kusini Riek Machar, huenda anaelekea kupata hifadhi nchini Afrika Kusini baada ya taifa hilo kukubali kumpokea kulingana na gazeti moja nchini Kenya.
Bwana Machar yuko mjini Khartoum baada ya kuondolewa kuhudumu kama makamu wa rais kufuatia ghasia zilizozuka mjini Juba kati ya vikosi vyake na vile vinavyomtii rais Salva Kiir.
Msemaji wa serikali nchini Kenya Manoah Esipisu aliliambia gazeti la Nation Jumapili kwamba Kenya ilishiriki katika mazungumzo ya ni wapi Machar anafaa kupewa hifadhi na kubaini kwamba Afrika Kusini iko tayari kumpokea.
Pia amesema kuwa makubaliano yaliafikiwa wiki iliopita ,kwa Kenya kutuma wanajeshi zaidi nchini Somalia kabla ya uchaguzi unaotarajiwa kufanyika kati ya Septemba 24 na Oktoba 10.
Esipisu alikuwa akijibu maswali kuhusu hatua ya rais Uhuru Kenyatta kuahirisha mipango yake ya kusafiri mjini New York ili kuhudhuria mkutano wa kila mwaka wa Umoja wa mataifa.
Alisema kwamba uwepo wa bwana Kenyatta ni muhimu katika kukabiliana na hali ya Somalia na ile ya Sudan Kusini.
Naibu wa rais William Ruto anamwakilisha rais Kenyatta katika mkutano huo wa UN.
Title :
Afrika Kusini ''yajitolea kumpatia hifadhi Riek Machar
Description : Aliyekuwa makamu wa rais nchini Sudan Kusini Riek Machar, huenda anaelekea kupata hifadhi nchini Afrika Kusini baada ya taifa hilo kukuba...
Rating :
5