Watu tisa wameuawa na wengine 10
kujeruhiwa baada ya watu wenye bunduki waliowafyatulia risasi watu
katika jumba moja la kibiashara mjini Munich, Ujerumani.
Polisi wanasema washukiwa bado hawajakamatwa na wamewatahadharisha watu na kuwashauri kutotoka nje.
Wanachunguza iwapo mmoja wa waliofariki ni mtuhumiwa.
Operesheni kubwa ya kiusalama inaendelea katika jumba la kibiashara
la Olympia, ambalo linapatikana mtaa wa Moosach, kaskazini magharibi mwa
Munich.
-
Merkel kukutana na wakuu wa usalama Ujerumani
-
Abiria washambuliwa kwenye Treni Ujerumani
Watu walioshuhudia tukio wanasema wamewaona watu watatu waliokuwa na bunduki.
Maafisa wa polisi jimbo la Bavaria wamekuwa katika
hali ya tahadhari tangu Jumatatu kijana mhamiaji alipowadunga visu na
kuwajeruhi watu kadha katika treni, shambulio ambalo kundi la Islamic
State lilidai kuhusika.
Polisi wamesema shambulio hilo ni la kigaidi.
-
Wakimbizi wamuokoa mwanasiasa Ujerumani
Wanasema habari
za kwanza kuhusu ufyatuaji wa risasi kwenye jumba hilo linalopatikana
katika barabara ya Hanauer zilitokea muda mfupi kabla ya saa thenashara
jioni.
Kituo kikuu cha treni katika mji huo wa Bavaria kimefungwa na watu kuondolewa.
Watu wengi wamekwama kutokana na kustishwa kwa
uchukuzi na kutokana na hali kwamba hawawezi kusafiri kurudi nyumbani,
wanapewa malazi ya wenyeji.
Kumeanzishwa kampeni kwenye Twitter inayotumia kitambulisha mada #Offenetür(fungua mlango).
Helikopta
za maafisa wa polisi zinapaa angani na maafisa maalum wa usalama
wanashiriki katika operesheni kubwa ya kuwasaka watuhumiwa.
Kituo
cha redio cha serikali ya Bavaria kimesema kikosi maalum cha polisi wa
mpakani kwa jina, GSG9, kinaelekea Munich kikitumia helikopta kadha.
Waziri mkuu wa Bavaria Horst Seehofer anaongoza mkutano wa dharura na washauri wa masuala ya usalama.
Jamhuri ya Czech, inayopakana na Ujerumani imeimarisha usalama mpakani.
Title :
WATU TISA 9 WAFARIKI KWENYE SHAMBULUO MINICH
Description : Watu tisa wameuawa na wengine 10 kujeruhiwa baada ya watu wenye bunduki waliowafyatulia risasi watu katika jumba moja la kibiashara mji...
Rating :
5