Jumamosi ya June 25 2016 mkuu wa idara ya habari na mawasiliano wa klabu
ya Dar es Salaam Young Africans Jerry Muro alitangaza viingilio vya
mechi yao ya Kombe la Shirikisho barani Afrika dhidi ya TP Mazembe
itakuwa na kiingilio kati ya Tsh 7000 hadi 30000.
Taarifa zilizotoka June 26 kuelekea mchezo huo wa pili wa Kundi A lenye
timu za MO Bejaia ya Algeria, TP Mazembe, Medeama ya Ghana na Yanga,
uongozi wa klabu ya Yanga wametangaza kuwa mechi yao wameamua mashabiki
waingie bure ili waweze kuishangilia timu yao.
Maamuzi hayo ya Yanga, wadau na mashabiki wa soka wanatafsiri kama ni
maamuzi ya hasira na yanatajwa kuja kutokana na TFF imewakosea kuingia
mkataba na Azam TV wa kurusha mechi hiyo live pasipo wao kushirikishwa,
wakati wao wanaamini kuwa mechi hiyo ikioneshwa Dar es Salaam watakosa
mapato.
Title :
MCHEZO KATI YA YANGA VS TP MAZEMBE KIINGILIO NI BURE....(SOMA ZAIDI)
Description : Jumamosi ya June 25 2016 mkuu wa idara ya habari na mawasiliano wa klabu ya Dar es Salaam Young Africans Jerry Muro alitangaza viingilio vy...
Rating :
5