Waziri wa mambo ya ndani nchini Tznania Charles Kitwanga amefutwakazi kutokana na sababu ya kuwa mlevi akiwa kazini.
Kwenye taarifa, rais John Magufuli alisema kuwa bwana Kitwanga alienda bungeni na kujibu swali la mbunge akiwa mlevi.
Hata hivyo bwana Kitwanga hajasema lolote.
Image copyright
Statehouse Tanzania
Image caption
Rais John Magufuli
Rais Magufuli ambaye aliingia ofisini mwaka uliopita
aliahidi kupambana na ufisadi na awewafuta kazi maafisa kadha kuhusiana
na suala la ufisadi.
Lakini waandishi wa habari wanasema kuwa
kufutwa kwa bwana Kitwanga ni jambo la kushangaza kwa sababu amekuwa
rafiki wa rais kwa siku nyingi