May 21 2016 Tanzania inaingia kwenye majonzi ya kumbukumbu ya kuzama meli ya Mv Bukoba ndani ya ziwa Victoria leo ni miaka 20 tangu meli izame Watanzania zaidi ya 1,000 walipoteza maisha.
Ibada ya kumbukumbu imefanyika leo kwenye makaburi ya Igoma Mwanza na kuhudhuriwa na Mwanamitindo wa Kimataifa Flaviana Matata ambaye ni miongoni mwa watu walipoteza wazazi wao, Mawaziri wa Serikali Nape Mnauye, January Makamba na Viongozi wengine wa Serikali pamoja na wananchi.

January Makamba, Wazari wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais, Muungano na Mazingira kwenye Ibada ya Kumbukumbu.

Nape Mnauye, Waziri wa Habari, Utamaduni Sanaa na Michezo nae alikuwepo.

Mkuu wa Wialaya ya Ilemela, Manju Msambya.

Waziri Nape, Makamba na Flaviana kwenye tukio la kuwasha mishumaa.

Viongozi wa Serikali kwenye tukio la kuweka Mashada

Mbunge wa Nyamagana Stanslaus Mabula nae alikuwepo kwenye kumbukumbu.

Mtangazaji wa Clouds Hamis Mandi (B dozen), nae alihudhuria Ibada

Waziri Nape na Flaviana Matata.

Waziri Makamba, Nape na Flaviana kwenye tukio la kuwasha mishumaa kwa pamoja.

Samweli Paschal Kijana aliyepoteza Wazazi wake wote yeye alinusurika.