R Kelly atuhumiwa kwa ''kuwanyanyasa kingono wanawake''
Mwanamuziki wa mtindo wa R&B R Kelly amekana madai kwamba anawazuia wanawake kadhaa katika dhehebu lake analotumia kuwanyanyasa.
Wakili wa mwanamuziki huyo alisema kuwa atatumia kila njia kuhakikisha kuwa wale wanaomtuhumu anawakabili kisheria ili kusafisha jina lake.
Ripoti ya BUzzFeed imemtuhumu mwanamuziki huyo kwa kuwabadili kimawazo wanawake walio karibu naye kwa lengo la kuimarisha usanii wao wa muziki.
Kelly tayari amewahi kukabiliwa na tuhuma za dhulma za kingono lakini hakupatikana na hatia.
Amekana kufanya makosa yoyote.
Ripoti hiyo iliowanukuu wazazi watatu inasema kuwa hawajawasiliana na wanao kwa miezi kadhaa ,na kwamba wanawake hao wote wakiwa na umri wa zaidi ya miaka 18 walikuwa wakidhibitiwa na msanii huyo.
Udhibiti huo unashirikisha chakula wanachokula na nguo wanazovaa ,wakati gani wa kuoga na kulala mbali na kufanya tendo la ngono yote hayo yakirekodiwa na msanii huyo.
Wanachama watatu walio karibu na mwanamuziki huyo pia walihojiwa na kusema kuwa wanawake sita wanaishi katika nyumba zinazosimamiwa na msanii huyo.
Iwapo watavunja sheria, wanasema wanawake hao huadhibiwa kwa kupigwa mbali na kutukanwa na msanii huyo kulingana na ripoti hiyo.
Baadhi ya wazazi wao wameripoti wasiwasi kwa polisi, lakini wanawake hao wanasema kuwa wamekubali kuishi katika nyumba hizo.
Wakili wa msanii huyo Linda Mesch alisema: Robert Kelly ameshangazwa na kukerwa kuhusu madai hayo mapya anayodai kutekeleza.
Title :
R Kelly Atuhumiwa Kwa ''Kuwanyanyasa Kingono Wanawake''
Description : R Kelly atuhumiwa kwa ''kuwanyanyasa kingono wanawake'' Mwanamuziki wa mtindo wa R&B R Kelly amekana madai kwamba a...
Rating :
5