Jumanne hii Leo jioni timu ya Gor Mahia imefanya mazoezi makali kwa muda wa Dakika 40 chini ya kocha wao mpya, Dylan Kerr huku kocha huyo akiwapigisha mazoezi ambayo hata wachezaji wenyewe wamekiri wazi kuwa ndoto za kuwagaragaza Everton zitatimia.
Kwenye mazoezi hayo Wachezaji wa Gor Mahia walionekana wenye nyuso za furaha huku wengi wakifurahia mandhari ya Uwanja na hali ya hewa ya jiji la Dar es salaam huenda ndoto yao ikatimia kwa kuwalaza Everton hiyo siku ya Alhamisi.
“Tunajua mchezo utakuwa mgumu lakini kwa mazoezi haya tunaamini tutawapa changamoto kwani hao wapo na wachezaji wageni wengi sisi tumekaa kwa muda mrefu tumezoeana,“amesema Kaptaini wa Gor Mahia, Musa Mohamed mapema baada ya kumaliza mazoezi.
Klabu ya Everton ipo njiani kuja Tanzania na inatarajiwa kutua nchini kesho asubuhi tayari kwa maandalizi ya kuvaana na Gor Mahia alhamisi hii (Julai 13)
Title :
Gor Mahia wafanya mazoezi ya kufa mtu: Waahidi kuwaangamiza Everton
Description : Jumanne hii Leo jioni timu ya Gor Mahia imefanya mazoezi makali kwa muda wa Dakika 40 chini ya kocha wao mpya, Dylan Kerr huku kocha huy...
Rating :
5