Mbunge wa jimbo la Mikumi Mh. Joseph Haule amefunguka na kuitaka serikali kuwekeza fedha za kutosha katika Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo ili wizara hiyo iweze kuwekeza katika sanaa na kuacha kuwatumia wasanii kama makarai ya kujengea.
Prof Jay alisema hayo Bungeni wakati akichangia makadilio ya mapato na matumizi ya Wizara ya Habari kwa mwaka 2017/ 2018
"Wasanii wa Tanzania wamekuwa katika mazingira magumu sana na wamekuwa katika umasikini mkubwa licha ya mara nyingi kutumiwa katika kampeni mbambali na hata katika chaguzi zilizopita mmeona jinsi wasanii walivyokuwa wakitumika, mmewatumia kama makarai na baada ya hapo mmeyaweka uvunguni, tunajua makarai huwa yanatumika kwenye kujenga maghorofa na vitu vingine lakini nyumba ikikamilika yanawekwa uvunguni hayatakiwa kuonekana hata kwa wageni" alisema Prof Jay
Mbali na hilo Prof Jay amesema wasanii wengi wa Tanzania wanakuwa masikini sana sababu wakishatumika huwa hawathaminiwa tena na kuachwa mpaka wakati mwingine wa uchaguzi au kampeni
By A lbert Luhogola
Title :
PROF Jay Awakilisha Kilio cha Wasanii Bungeni..Aichoma Mkuki wa Moyoni CCM ..!!!
Description : Mbunge wa jimbo la Mikumi Mh. Joseph Haule amefunguka na kuitaka serikali kuwekeza fedha za kutosha katika Wizara ya...
Rating :
5