Producer mkongwe wa muziki wa Bongo Fleva nchini Tanzania, P-Funk Majani ameshindwa kujizuia kummagia sifa Rapa Fid Q kwa kusema kuwa ni Msanii mbunifu sana na mwenye misimamo.
P-Funk amesema Fid Q ni Msanii mwenye misimamo na hajawahi kubadilika kufuata upepo wa muziki bali mara zote husimamia misingi ya hip hop na kila siku unamuona mpya .
“Unapomzungumzia Fid Q ni full package kwa sababu ni mbunifu na mashairi anayo ya kutosha, haigilizii kutoka kwa msanii yoyote kutoka nje lakini hajawahi kubadilika kutokana na upepo wa game. Kila mara unapomuona Fid utaona kuna vitu vinaongezeka kwake lakini vya kipekee kabisa. Kuna wasanii wanaofanya vizuri lakini ukisikiliza mashairi yao huelewi ila Fid licha ya kuwa na ladha nzuri ya sauti ya muziki lakini mashairi yake yatakufanya useme huyu ni msanii Full Package”Alisema P-Funk Majani kwenye mahojiano yake na East Africa Radio.
Hata hivyo P-Funk Majani anaamini kuwa wasanii wengi hususani Marapa wamekuwa wakibadilika kila siku kwa kuiga Marapa wa nje kitu ambacho kinawafanya wakose soko.
Title :
Fid Q ni ‘full package’ – P-Funk Majani
Description : Producer mkongwe wa muziki wa Bongo Fleva nchini Tanzania, P-Funk Majani ameshindwa kujizuia kummagia sifa Rapa Fid Q kwa kusema kuwa...
Rating :
5