Kila siku asubuhi huwa nazisogeza headlines zilizobebwa kwenye kurasa za Magazeti ya Tanzania, Uchambuzi wa stori zote napandisha kwenye account yangu ya Twitter>>>@millardayo na Zote nakusogezea hapa chini
Moja ya story kubwa June 02 2016 kwenye gazeti la Mwananchi ni hii yenye kichwa cha habari ‘watakaogonga mabasi ya Udart faini 300,000‘
Gazeti la
Mwananchi limeripoti kuwa madereva wa magari, bodaboda na bajaji
wanaovunja sheria na kuyasababisha ajali ya mabasi ya haraka watatozwa
faini isiyopungua sh 300,000.
Gazeti hilo limezungumza meneja
uhusiano wa Dart, William Gatambi ambaye amesema wamewasilisha maoni ya
kupitishiwa sheria ndogondogo kwa ajili ya barabara zinazotumiwa na
mabasi hayo katika wizara husika kwa ajili ya kufanyiwa kazi