WACHIMBAJI wadogo wadogo wa dhahabu wa mgodi ulioko katika kijiji cha
Nyasana kata ya Kabasa Wilaya ya Bunda, mkoani Mara wameshauriwa
kujiunga kwenye ujasiriamali ili halmashauri ya Mji wa Bunda na
serikali kwa ujumla iweze kuona namna ya kuwawezesha ili wajiinue
kiuchumi.
Ushauri huo umetolewa na mwenyekiti wa halmashauri ya Mji wa Bunda,
Abrahamu Mayaya, wakati akifungua ofisi ya kijiji hicho, ikliyojengwa
kwa mchango mkubwa uliotolewa na wachimbaji wadogo wadogo, kwa
kushirikiana na wananchi wa kijiji hicho kwa thamani ya zaidi ya
shilingi milioni 9.5.
Mheshimiwa Mayaya ambaye pia ni diwani wa kata hiyo, amesema kuwa
serikali inatambua mchango mkubwa unaofanywa na wachimbaji wadogo
wadogo, katika suala zima la kuchangia miradi ya maendeleo na akawaomba
wachimbaji hao wajiunge kwenye vikundi vya ujasiriamali ili waweze
kujiinua kiuchumi.
Amesema kuwa kutokana na wachimaji hao kuchangia miradi mbalimbali ya
maendeleo, halmashauri ya Mji wa Bunda pamoja na serikali kwa ujumla,
itafanya kila liwezekanalo kwa kuunga mkono juhudi za wananchi hao,
ikiwa ni pamoja na kujenga zahanati kijijini hapo ili wananchi waweze
kupata huduma za amatibabu kwa ukaribu zaidi.
Hata hivyo anasisitiza viongozi kujenga tabia ya kuwasomea wananchi
mapato na matumizi juu ya miradi mbalimbali ya maendeleo inayotekelezwa
katika maeneo yao.
Mwenyekiti wa kijiji hicho Dismas Mathindo, anasema kuwa katika
ujenzi wa ofisi hiyo wachimbaji wadogo wadogo katika mgodi huo,
wamechangi kwa kiasi kikubwa.
Makamu mwenyekiti wa wachimbaji wadogo wadogo katika Wilaya ya Bunda,
Georges Miyawa na mwenyekiti wa wachimbaji hao katika mgodi huo Justine
Raphael, wanaiomba serikali kusaidia kuondoa changamoto zinazowakabili
wachimbaji hao, kwani ni wadau wakubwa katika suala zima la kuchangia
miradi ya maendeleo.
Title :
WACHIMBAJI WAMIGODI WAZIDI KUONGEZEKA MIGODINI GEITA....(SOMA ZAIDI)
Description : WACHIMBAJI wadogo wadogo wa dhahabu wa mgodi ulioko katika kijiji cha Nyasana kata ya Kabasa Wilaya ya Bunda, mkoani Mara wameshauriwa k...
Rating :
5