Baadhi ya wakazi wa jiji la Dar Es Salaam wameziomba mamlaka
zinazohusika na uratibu wa usafiri wa mabasi yaendayo haraka jijini
humo, kutafuta ufumbuzi wa matatizo yaliyojitokeza katika mfumo wa
ukataji tiketi ikiwemo upatikanaji wa chenji na mashine kwa ajili ya
kuhakiki tiketi.
Wakizungumza na TBC kwa nyakati tofauti, wakazi hao wamesema wanapata
usumbufu kwa kutumia muda mwingi kuhakiki tiketi huku wengine
wakilazimika kusubiri kwa muda mrefu wakati wakitafutiwa chenji.
Mradi wa mabasi yaendayo haraka ulizinduliwa wiki iliyopita ambapo
wananchi walipata fursa ya kutumia usafiri huo bila malipo na kuanzia
Jumatatu wiki hii wameanza kulipia gharama za usafiri huo.
Title :
NEW:MABASI MWENDO KASI DAR YAANZA KABAKOO....(SOMA ZAIDI)
Description : Baadhi ya wakazi wa jiji la Dar Es Salaam wameziomba mamlaka zinazohusika na uratibu wa usafiri wa mabasi yaendayo haraka jijini humo, k...
Rating :
5